1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pengo la ujuzi wa historia ya Ujerumani

5 Novemba 2009

Chipukizi kati ya umri 15-17 wana kasoro hiyo.Miaka 20 tangu kuporomoka kwa ukuta wa Berlin, wanafunzi wa Ujerumani, wana kasoro kubwa katika kuielewa historia ya iliokuwa Ujerumani Mashariki (GDR).

https://p.dw.com/p/KHUl
Ukuta wa Berlin ulijengwa lini ?Picha: Andrzej Stach

Hayo ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha (Free University ) mjini Berlin kuhusu sura walionayo wanafunzi chipukizi kati ya umri wa miaka 15 hadi 17.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani (GDR) anaitwaje ?

Mngali mnakumbuka ? .......anaitwa Willy Brandt ? Sio....Erich Honecker ? Ndio, ni Erich Honecker.

Hali kama hiyo ya kutofahamu historia inawakuta zaidi ya vijana 5000 walioulizwa maswali katika uchunguzi huo. Mtaalamu wa fani ya siasa Klaus Schroeder anafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Free University mjini Berlin na ndie alieongoza uchunguzi huo: Bw.Schroeder asema,

"Bila kujali aina ya shule,asili ya mwanafunzi na hata umri, kila mkoa wa shirikisho hali ni sawa sawa.Kwa jinsi mtu anavyofahamu zaidi, ndivyo Ujerumani Mashariki (GDR) inavyoeleweka ulikuwa utawala wa kidikteta.Na wale wasiojua mengi,hawajui wasimame wapi au huwa na sura njema juu yake.Kutokana na hali hiyo, tumeona ikiwa wanafunzi wataelimishwa barabara zaidi na wakielewa zaidi hasa huko mashariki mwa Ujerumani,watabadili sura na maoni yao juu ya Ujerumani Mashariki (GDR) ilivyokuwa."

Katika Ujerumani Magharibi kila mwanafunzi 3 na huko mashariki kila wapili,hawaiangali Ujerumani Mashariki kuwa ulikuwa ni utawala wa kidikteta.

Katika mkoa wa shirikisho wa Brandenburg ,hawaioni ile ilikuwa "Idara ya usalama wa taifa" iliogopwa (STASI) kuwa na dhara yoyote mbali na kuwa idara ya usalama ya kawaida kama zilivyo nyengine katika nchi nyengine.

Ujuzi wa chipukizi katika mkoa wa Ujerumani Magharibi wa Northrhein-westfalia na wa kusini wa Bavaria si bora hivyo kuliko ule wa wenzao wa mashariki.Ni wanafunzi wachache tu wanaojua kuwa, hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980 katika Ujerumani Mashariki kulikuwa na adhabu ya kifo.Hawajui pia juu ya mateso na madhila ya kila siku ,vyombo vya dola vilivyo wachunguza watu , juu ya magereza maalumu na wakimbizi katika ukuta wa Berlin.

Mwanafunzi mmoja anajibu kuwa, ukuta wa Berlin uliojengwa August 13,1961, eti ulijengwa 1940.Sijui barabara,nadhani tu ni hivyo. Wengine wakihusudu kuwa chipukizi katika iliokuwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani wakiendelezwa mno katika fani ya spoti.

Kila mwanafunzi wa 3 amewataja viongozi 2 mashuhuri wa serikali ya Ujerumani magharibi Konrad Adenauer na Willy Brandt kuwa ni wanasiasa wa Ujerumani Mashariki.54% ya wanafunzi mkoani Brandenburg, hawakujua tarehe ya kujengwa ukuta wa Berlin-August,13,1961.

Chanzo cha kutojua vya kutosha historia yao, hakipo kwa muujibu wa Bibi Monika Deutz-Schroeder, katika mpango wa mafunzo ,bali hata sehemu ya walimu hawajui mengi juu ya maswali ya kimazingira.

Mtayarishi: Mareka,Michael /ZR/Ramadhan Ali

Mhariri: Abdul-Rahman