1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pendekezo la nyongeza ya asilimia 13 kwa madereva wa treni

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSqT

Shirika la reli la Ujerumani-Deutsche Bahn limesema,limetoa pendekezo kwa chama cha wafanyakazi cha madereva wa treni GDL,kuongeza mshahara wao hadi asilimia 13,katika juhudi ya kutaka kumaliza mgogoro wa majuma kadhaa.

Viongozi wa GDL watakutana siku ya Jumatatu kuamua iwapo washiriki katika majadiliano rasmi kuhusu pendekezo hilo jipya.Migomo iliyofanywa na madereva wa treni wa GDL katika majuma yaliyopita ilivuruga huduma za usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo.Inatathminiwa kuwa migomo hiyo,imesababisha hasara ya mamilioni ya Euro katika uchumi wa Ujerumani.