1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pendekezo la kupeleka vikosi zaidi Afghanistan

11 Februari 2010

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amewasilisha bungeni mjini Berlin mkakati mpya wa serikali kuhusu Afghanistan.

https://p.dw.com/p/Lyaq
Bundesaußenminister Guido Westerwelle (FDP) gibt am Mittwoch (10.02.2010) im Bundestag in Berlin eine Regierungserklärung zur neuen Afghanistan-Strategie ab. Daran schließt sich die erste Beratung des vom Kabinett beschlossenen Entwurfs für ein neues Mandat an, das die Aufstockung des Bundeswehrkontingents in der internationalen Schutztruppe von 4500 auf bis zu 5350 Soldaten vorsieht. Foto: Arno Burgi dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle katika Bunge la Ujerumani-Bundestag.Picha: picture alliance/dpa
Mkakati huo unapendekeza kupeleka wanajeshi zaidi nchini humo na kutilia mkazo kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan. Waziri Guido Westerwelle akiupigia upatu mpango huo,alizungumzia makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu Afghanistan uliofanywa mjini London mwishoni mwa mwezi wa Januari. Kuambatana na makubaliano hayo, ujenzi mpya na mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan yapewe kipaumbele. Hata hivyo amesema kuna baadhi ya mambo yaliyoweza kutekelezwa. Kwa mfano, kumejengwa shule nyingi mpya,wenyeji wamepatiwa maji na umeme na kuna maendeleo katika sekta ya kilimo pia. Lakini pia kulikuwepo matokeo yasiyofurahisha. CLIP:WESTERWELLE: "Mwaka uliopita hali ya usalama ilichafuka upya. Bado kama asilimia 90 ya kasumba katika masoko ya dunia inatoka Afghanistan. Hali inayokutikana leo hii nchini Afghanistan si ile tuliyotazamia miaka minane iliyopita.Kwa hivyo serikali hii ya Ujerumani tangu mwanzoni imeshughulikia mkakati mpya." Si kwamba anakosoa mkakati uliokuwa ukifuatwa na serikali iliyotangulia bali kumepatikana somo muhimu kutoka yale yaliyotokea miaka iliyopita aliongezea waziri wa nje wa Ujerumani. Ni matumaini yake kuwa ifikapo mwaka 2011,vikosi vya Afghanistan vitaweza kukabidhiwa jukumu la kulinda usalama hatua kwa hatua na majeshi ya Ujerumani kuanza kurejea nyumbani. Utaratibu huo unatazamiwa kukamilishwa mwaka 2014. Amesema hivyo ndio inavyotazamiwa lakini hiyo si tarehe maalum iliyopangwa kuondoka Afghanistan. Itakuwa kosa kupanga wakati maalum wa kuondoka kwani hiyo itawapa moyo magaidi. Mkakati mpya wa Ujerumani unaopigiwa upatu bungeni na waziri Westerwelle unapendekeza kupeleka wanajeshi 850 zaidi na kipaumbele ni kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan. Ujerumani tayari ina wanajeshi wapatao 4,500 nchini Afghanistan. Serikali ya Kansela Angela Merkel inapanga pia kuongeza msaada wa maendeleo nchini Afghanistan kwa takriban maradufu na hivyo kufikia Euro milioni 430. Mkakati huo mpya uliungwa mkono na baraza la mawaziri Jumanne iliyopita na sasa bunge kuu la Ujerumani Bundestag linangojewa kutoa idhini yake hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Februari. Mwandishi: Fürstenau,Marcel/ZPR/P.Martin Mpitiaji: Aboubakary Liongo