1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pele aondoka hospitalini baada ya upasuaji

9 Mei 2015

Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya kandanda ya Brazil Pele ameruhusiwa kuondoka hospitalini mjini Sao Paulo baada ya kupata nafuu kutokana na upasuaji wa kibofu cha mkojo

https://p.dw.com/p/1FNJO
Brasilien Fußball Pele
Picha: picture-alliance/dpa/B. Zborowski

Pele mwenye umri wa miaka 74 alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Albert Einstein, mjini Sao Paulo, ambako pia alitibiwa mwaka jana kutokana na matatozo ya njia ya mkojo. Hospitali hiyo imesema katika taarifa kuwa nguli huyo wa kandanda anaendelea vyema, bila kutoa maelezo zaidi. Pele alilazwa katika hospitali hiyo takriban miezi sita iliopita kwa upasuaji wa dharura ili kuondoa mawe katika figo yake.

Pele aliifungia Brazil zaidi ya mabao 1,200 wakati alipokuwa akicheza soka na kuisaidia kushinda mataji matatu ya kombe la dunia. Kwa sasa ni balozi wa mchezo wa kandanda ulimwenguni.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu