1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Upinzani wajikakamua kupata ushindi

11 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsh

Chama tawala cha mrengo wa kulia cha UMP cha Rais Nikolas Sarkozy kimepata ushindi mkubwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge hapo jana.Ushindi huo unamwezesha kufanya mabadiliko nchini Ufaransa.Hatua hiyo inatarajiwa kuwezesha chama cha UMP kupata viti 501 kati ya 577 katika bunge.

Chama cha UMP kwa sasa kina viti 359 katika bunge dogo.

Waziri mkuu wa Ufaransa Francois Fillon anatoa wito kwa raia wa Ufaransa kujitokeza kwa wingi jumapili ijayo ili kupiga kura.

Chama cha UMP cha Rais Nikolas Sarkozy kina umaarufu mkubwa tangu kujinyakulia ushindi na kuahidi kuimarisha uchumi,kudhibiti sheria za uhamiaji vilevile kupambana na uhalifu.

Kwa upande mwingine chama kikuu cha upinzani cha Socialist cha Bi Segolene Royal aliyeshindwa katika uchaguzi wa Rais kinadhaniwa kuwa kitapoteza viti katika bunge.Kwa mujibu wa kura za maoni chama cha Socialist huenda kikapoteza zaidi ya nusu ya viti vyake 149 bungeni.