PARIS:Sarkozy aimarisha utawala wake | Habari za Ulimwengu | DW | 18.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS:Sarkozy aimarisha utawala wake

Chama cha kihafidhina cha rais Nicolas Sarkozy kimeshinda katika raundi ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini Ufaransa.Lakini hakikupata kura nyingi sana kulingana na utabiri wa hapo awali.Chama cha kisoshalisti pia kilifanya vizuri katika uchaguzi huo.

Wakati huo huo aliekuwa mgombea wa kiti cha urais kutoka chama hicho cha kisoshalisti bibi Segolene Royal amesema kuwa ametengana na mumewe bwana Francois Hollande baada ya kuishi pamoja kwa muda wa miaka 30.

Bibi Royal amethibitisha habari hizo na amesema kuwa atatoa taarifa rasmi baadae leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com