1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Rais wa Ufaransa ziarani nchini Libya

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfa

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa anakwenda Libya hii leo, katika mikakati ya kuirejesha Libya katika uhusiano na nchi za magharibi na pia kuimarisha maslahi ya Ufaransa katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.

Hapo jana Libya iliwaaruhusu wauguzi sita wa Bulgaria waliyokuwa wakitumikia kifungo cha maisha kwa kosa la kuwaambukiza watoto virusi vya HIV kutumikia kifungo nchini kwao.

Hiyo ilikuwa baada ya kufikiwa kwa makubaliano na Umoja wa Ulaya, katika majadiliano yaliyomshirikisha mke wa rais wa Ufaransa aliyekwenda Libya.

Wauguzi hao mara baada ya kuwasili Bulgaria walipewa msamaha na rais wa nchi hiyo.

Kiongozi huyo wa Ufaransa, amesema kuwa anataka kuisadia Libya kurejea katika ulimwengu wa mataifa mengine baada ya kutengwa kwa zaidi ya miongo mitatu kutokana na madai ya nchi za magharibi kuwa inafadhili vikundi vya kigaidi.