1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Rais Denis Sassou Ngweso aonya juu ya mzozo wa Sudan

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsZ

Mwenyekiti wa umoja wa nchi za Afrika rais Denis Sassou Ngweso wa Kongo Brazaville ameonya kuwa mzozo wa Sudan huenda ukatapakaza machafuko katika eneo zima la Afrika.

Wakati huo huo rais Ngweso ameutaka umoja wa mataifa upeleke jeshi la kulinda amani katika mipaka ya Chad na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Rais Ngweso aliyasema hayo mjini Paris baada ya kumaliza mkutano wake na rais Jaque Chirac wa Ufaransa.