1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Nicolas Sarkozy ajiuzulu wadhfa wake

26 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFD

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amejiuzulu wadhfa wake ili ashughulikie kampeni za uchaguzi wa rais uliopangiwa kufanyika mwezi ujao.

Francois Baroin amepewa wadhfa huo wa uwaziri wa mambo ya ndani baada ya kujiuzulu Sarkozy mwenye umri wa miaka 52 na anaetarajia kugombea kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha kihafidhina cha UMP.

Bwana Baroin hadi kupewa wadhfa huo mpya amekuwa ni waziri wa uhusiano wa Ufaransa na nchi zilizo chini ya himaya yake.

Ijapokuwa Nicolas Sarkozy anaongoza katika kura ya maoni dhidi ya bibi Segoline Royal na mgomea mwingine wa chama cha mlengo wa kadiri Francois Bayrou lakini matokeo ya hivi punde yanaonyesha kuwa umaarufu wa Sarkozy umepungua katika wiki chache za hivi karibuni.