1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Waziri mkuu ashutumu shambulio dhidi ya basi.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy4

Waziri mkuu wa Ufaransa Dominique de Villepin ameshutumu shambulio lililofanywa na wahuni dhidi ya basi moja katika mji wa kusini wa Marseille ambalo limesababisha kupata majeraha ya kuungua kwa mwanamke mmoja akiwa katika hali mbaya sana.

Polisi wamesema kuwa abiria wengine watatu wametibiwa kutokana na kuvuta hewa chafu ya moshi.

Shambulio hilo limekuja wakati Ufaransa imekuwa ikiadhimisha mwaka mmoja tangu kutokee machafuko ambayo yameyakumba maeneo mengi ya masikini nchini humo, yanayoishi wahamiaji.

Wahuni walichoma moto kiasi mabasi saba katika vitongoji kuzunguka mji wa Paris katika muda wa wiki moja iliyopita katika hali ya kupanda tena kwa machafuko kabla ya maadhimisho hayo, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo.