1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ufaransa yajaribu kombora la masafa marefu

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuT

Ufaransa imefanya jaribio la kombora jipya aina ya M-51 lenye uwezo wa kwenda umbali wa kilomita 6,000.Kombora hilo linaweza kupachikwa mabomu sita ya kinuklia.Kuanzia mwaka 2010,makombora ya aina hiyo,yatachukua nafasi ya makombora yanayotumiwa hivi sasa katika nyambizi.Jaribio hilo lilifanywa kwenye ghuba ya Biscay,nje ya mwambao wa Ufaransa kwenye bahari ya Atlantik. Polisi walilinda eneo hilo ili kuwazuia wanamazingira kuingilia kati.