PARIS : Taasisi za magharibi zakata uhusiano na ile ya Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS : Taasisi za magharibi zakata uhusiano na ile ya Iran

Takriban taasisi za utafiti 40 za Ulaya na Marekani ya Kaskazini zimesema kwamba zinasitisha mawasiliano na jopo kuu la ushauri la Iran ambalo limesaidia kuandaa mkutano wa wiki iliopita mjini Tehran wa watu wanaokanusha Maangamizi ya Wayahudi. Taasisi hizo zimekubali kusitisha mipango inayoendelea kutekelezwa na Taasisi ya Masomo ya Kisiasa ya Kimataifa ya Iran.

Mkutano uliofanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu wa Desemba mjini Tehran uliwajumuisha pamoja watu wanaokanusha Maangamizi ya Wayahudi kutoka duniani kote kujadili iwapo au la mauaji ya kimbari ya Wayahudi milioni sita yametokea kweli wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com