1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Sarkozy yu ziarani Russia.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HN

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anakwenda mjini Moscow leo ambako anatarajiwa kujenga ushirika mpya na Russia, nchi ambayo amekuwa akiishutumu kwa kuleta mkanganyiko katika masuala ya dunia.

Mkutano huo wa kwanza muhimu wa Sarkozy na Vladimir Putin unaweza kuzusha mvutano kwasababu tangu kuchaguliwa kwake May mwaka huu, amekuwa akiishambulia rekodi ya haki za binadamu ya Russia na kuishutumu kwa kutumia utajiri wake mkubwa wa gesi na mafuta kwa kuwaburuza majirani zake wa Ulaya, wakati akitaka uhusiano mwema na Marekani. Katika ziara yake mjini Sofia, Bulgaria wiki iliyopita , Sarkozy ameishutumu Russia kwa kupinda matatizo ya dunia, akisema kuwa nchi hiyo inapaswa kutambua kuwa nchi zenye nguvu sio tu zina haki, lakini pia zinamajukumu.