1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy na Royal waendelea na kampeni

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7S

Mgombea urais wa chama cha mrengo wa kati na kulia, Nicolas Sarkozy, na mgombea wa chama cha Soacialist, Ségoléne Royal, wananafanya kampeni za kujipatia kura huku duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Ufaransa ikikaribia kufanyika katika siku 12 zijazo.

Nicholas Sarkozy amesema atajaribu kuwavutia wapigaji kura katika nyanja zote za kisiasa. Mshauri wake, Axel Poniatowski, amesema atazungumzia kuhusu jamii ya undugu kwa Wafaransa.

´Alikuwa akizungumza kuhusu jamii ya undugu ambayo nadhani ni maneno mazito. Na huu ndio ujumbe atakaouzungumza kwa Wafaransa kuanzia sasa.´

Ségoléne Royal kwa upande wake amesema anataka kufanya mdahalo na mgombea wa chama cha mrengo wa kati, Francois Bayrou, aliyeshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Kura ya maoni imebashiri kuwa Sarkozy huenda akashinda baada ya kupata ushindi mkubwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi juzi Jumapili.