1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy azuru Libya

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfN

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ameondoka leo mjini Paris kwenda Tripoli Libya kituo chake cha kwanza katika ziara yake barani Afrika.

Rais Sarkozy anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Libya, kanali Muamar Gaddafi.

Rais Sarkozy alitangaza atafanya ziara yake ya kisiasa nchini Libya baada ya juhudi za Ufaransa kuchangia katika kuachiliwa huru wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa kipalestina.

Wataalamu hao wa afya walikuwa wakizuiliwa nchini Libya tangu mwaka wa 1999 kwa madai kwamba waliwaambukiza watoto zaidi ya 400 virusi vya ukimwi katika hospitali ya Bengazi.

Wachambuzi wanasema Libya, yenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi, huenda ikawa mshirika muhimu wa kibiashara wa Ufaransa.