1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy apumzika kabla ya kushika wadhifa mpya

8 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3x

Rais mteule wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy amewasili kisiwani Malta kwa mapumziko ya siku chache kabla ya kuchukua rasmi madaraka ya urais hapo tarehe 16 mwezi huu.Msemaji wa Sarkozy ameeleza kuwa mwanasiasa huyo wa kihafidhina aliekuwa waziri wa mambo ya ndani,atatumia muda huu kuchagua baraza lake la mawaziri.Hapo awali,Sarkozy aliahidi kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kisiasa. Wakati huo huo alitoa mwito wa kuwepo maridhiano baada ya kumshinda mpinzani wake wa chama cha Kisoshalisti Bibi Segolene Royal.Kwa upande mwingine kwa usiku wa pili kwa mfululizo,vijana wanaompinga Sarkozy,wameandamana katika miji mbali mbali nchini Ufaransa.Mjini Paris,polisi wamewakamata watu 35 baada ya kuzuka ghasia za kuvunja madirisha na kuharibu magari.