1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Rais Sarkozy ameahidi enzi mpya

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1P

Enzi mpya imefunguliwa nchini Ufaransa baada ya mhafidhina Nicolas Sarkozy kumpokea Jacques Chirac madaraka ya urais katika sherehe iliyofanywa mji mkuu Paris.Mhafidhina Sarkozy aliemshinda Segolene Royal wa chama cha Kisoshalisti katika uchaguzi wa tarehe 6 Mei ameahidi kuiongoza Ufaransa katika enzi mpya ya mageuzi.Rais Sarkozy anatarajiwa Berlin,mji mkuu wa Ujerumani,baadae leo hii ambako atakutana na Kansela Angela Merkel.Katika mkutano huo Sarkozy atasisitiza umuhimu wa uhusiano wa Ufaransa na Ujerumani.Jacques Chirac,mwenye umri wa miaka 72 ameondoka madarakani baada ya kuwa rais wa Ufaransa kwa miaka 12.