1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Polisi Ufaransa wapambana na waandamanaji

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4E

Nchini Ufaransa polisi wa kuzuia ghasia wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji kwenye uwanja wa Bastille mjini Paris,baada ya Nicolas Sarkozy wa chama cha kihafidhina kushinda uchaguzi wa rais nchini humo.Polisi walipambana na wafanya ghasia mjini Paris na katika miji mingine mbali mbali,baada ya kudhihirika kwa matokeo ya uchaguzi huo.Maandamano ya kumpinga Sarkozy yalifanywa pia katika miji kama Lyon, Marseilles,Toulouse na Lille.Kwa mara nyingine tena wafanya ghasia walichoma moto magari.Wakati wa kampeni za uchaguzi,Wasoshalisti walioshindwa uchaguzi wa siku ya Jumapili,walionya kuwa mivutano huenda ikaongezeka katika mitaa wanapoishi watu wa makabila mbalimbali,pindi Sarkozy atachaguliwa.Mnamo mwaka 2005,machafuko makubwa yalitokea katika maeneo hayo.