1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Msoshalist ateuliwa kuwa mkurugenzi wa IMF.

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBky

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amemteua waziri wa zamani wa fedha kutoka chama cha upinzani cha Kisoshalist kuliongoza shirika la fedha la kimataifa IMF.

Sarkozy amesema kuwa Dominique Strauss-Kahn anafaa zaidi kushika wadhifa huo wa mkurugenzi wa IMF.

Wadhifa huo utakuwa wazi hivi karibuni baada ya mkuu wa sasa wa shirika hilo Rodrigo Rato kutoka Hispania kutangaza kuwa atajiuzulu kabla ya muda wake kumalizika .

Kwa kawaida , mataifa ya ulaya yanamteua mkurugenzi mtendaji wa shirika la IMF na Marekani inachukua wadhifa wa rais wa benki ya dunia.