1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Fillon waziri mkuu Ufaransa

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1E

Rais Sarkozy leo hii amemtangaza muhafidhina mwenye mtizamo wa mageuzi Francois Fillon kuwa waziri mkuu mpya wa Ufaransa.

Fillon mwenye umri wa miaka 53 alipanga kampeni ya Sarkozy na alishirikiana na vyama vya wafanyakazi vyenye nguvu kubwa kushinikiza mageuzi nyenti na kumfanya astahiki kuwa chaguo la kushika wadhifa huo kuongoza mabadiliko juu ya sheria za kazi na mfumo wa malipo ya uzeeni wa Ufaransa ulio na ukarimu.

Fillon yumkini akatangaza serikali yake mpya hapo kesho.