1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Chiran kung’atuka madarakani.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJs

Rais wa Ufaransa Jacques Chirac amethibitisha kuwa hatagombea tena kipindi kingine cha urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao.

Katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya televisheni kwa taifa , Chirac alifanya majumuisho ya kile anachokiona kuwa ni mafanikio ya utawala wake wa miaka 12, ikiwa ni pamoja na hali bora kwa wazee na walemavu, mageuzi katika mfumo wa akiba ya uzeeni na kupungua kwa uhalifu na ukosefu wa nafasi za kazi. Chirac amesema.

Chirac ataondoka rasmi madarakani katika mwezi wa May baada ya kushughulika kisiasa kwa muda wa miaka 40. Uchaguzi wa rais unatarajiwa kufanyika katika duru mbili za upigaji kura hapo Aprili 22 na May 6. Kura za maoni zinaelekeza katika mpambano kati ya Nikolas Sarkozy anayefuata mrengo wa kulia na msoshalist Segolene Royal pamoja na Francois Bayrou wa mrengo wa kati.