1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Bayrou awashutumu wagombea urais

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC77

Ikiwa imebakia wiki moja na nusu kabla ya kufanyika kwa marudio ya uchaguzi wa rais nchini Ufaransa mgombea wa sera za wastani Francois Bayrou anagoma kuwaunga mkono wagombea wote wawili mhafidhina Nicolas Sarkozy na msoshalisti Segolene Royal.

Bayrou ambaye ameshika nafasi ya tatu katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini humo amesema kwamba wagombea hao wote wawili wataizidishia tu matatizo Ufaransa. Amesema anahofu kwamba Sarkozy atazidisha mvutano wa kijamii nchini Ufaransa wakati Royal anaweza kuyafanya matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo kuwa mabaya zaidi.

Sarkozy na Royal wote wawili wamekuwa wakiwanyatia wapiga kura wa sera za wastani kwa ajili ya marudio ya uchaguzi huo wa rais uliopangwa kufanyika hapo tarehe 6 mwezi wa Mei ambapo Sarkozy kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni anaongoza kwa kati ya asilimia mbili na saba.