1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis Yuko Uganda

28 Novemba 2015

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis atatoa heshima zake kwa Wakristo wa karne ya 19 nchini Uganda ambao walichomwa moto wakiwa hai wakigoma kuikana imani yao.

https://p.dw.com/p/1HDtS
Uganda Papst Franziskus mit Präsident Yoweri Museveni
Papa Francis akikaribishwa nchini Uganda na rais Yoweri MuseveniPicha: Reuters/J. Akena

Hilo ni kundi la hivi karibuni kabisa la mashahidi kutoka duniani kote walioadhimishwa na papa Francis kwa matumaini ya kuwapa mfano waumini wa umisionari wa hivi sasa .

Francis atasali leo Jumamosi katika eneo la ibada lililotengwa kwa ajili ya mashahidi Waanglikana 23 na Wakatoliki 22 ambao waliuwawa kati ya mwaka 1885 na 1887 kwa amri ya mfalme wa eneo hilo ambaye aliazimia kuzuwia ushawishi wa Ukristo katika ufalme wake katikati mwa Uganda.

Uganda Papst Franziskus
Mabango makubwa yakimkaribisha kiongozi huyo wa kanisa KatolikiPicha: Reuters/E. Echwalu

Katika eneo la Namugongo, ambako wengi wa mashahidi hao wa Uganda walichomwa moto wakiwa hai, ataongoza misa kwa heshima ya mashahidi hao katika kumbukumbu ya miaka 50 ya kanuni za madhehebu ya Katoliki.

Zaidi ya watu milioni mbili wanatarajiwa kuhudhuria, ikiwa ni pamoja na rais wa nchi jirani ya Sudan kusini, ambaye pia amekutana pia na papa Francis kwa faragha baada ya sherehe rasmi za kumkaribisha Jumamosi na rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Umuhimu wa imani

"Wanatukumbusha kuhusu umuhimu wa imani, usahihi wa kimoyo na nia thabiti kuelekea kile waliochokilenga kwa pamoja, na kinachoendelea hadi sasa, katika maisha ya utamaduni , uchumi na kisiasa katika nchi hii," Francis amemwambai rais Museveni na maafisa wengine wa Uganda pamoja na wanadiplomasia katika sherehe zilizofanyika katika Ikulu ya Uganda.

Baada ya sherehe hizo, Papa Francis alikaribishwa katika eneo la pili la ibada kwa mashahidi hao na mamia kwa maelfu ya waumini pamoja na wacheza ngoma za kienyeji , ikiwa ni ushahidi wa hamasa waliyonayo Waganda kwa ujio wa papa Francis katika ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika.

Wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini Uganda, Francis anatarajiwa kugusia baadhi ya mada zile zile alizosisitiza wakati wa sehemu ya kwanza ya ziara yake nchini Kenya: rushwa, umasikini na kuwapa matumaini vijana wa kikristo na matumaini. Baada ya misa leo Jumamosi(28.11.2015), Francis atakuwa na mkutano na vijana, ziara katika shirika la kutoa misaada na mkutano na makasisi wa nchi hiyo, waseminari na watawa.

Uganda Papst Franziskus
Mwanamke wa Uganda akishikilia picha ya papa FrancisPicha: Reuters/E. Echwalu

Ukarabati eneo la Namugongo

Katika matayarisho ya ziara yake, wafanyakazi wamekuwa wakijishughulisha sana usiku na mchana wakitengeneza barabara nyembamba inayoelekea katika eneo la ibada la Namugongo. Eneo hilo binafsi limefanyiwa ukarabati mkubwa ambao umefanywa kama mradi wa kijeshi.

Wanajeshi wa kikosi cha uhandisi cha brigedi ya jeshi la Uganda walijiunga na mkandarasi kufanya kazi tangu kupanda nyasi hadi kuweka changarawe.

Francis ameahidi katika ziara zake za nje kutoa heshima kwa mashahidi wa kila nchi kwa matumaini ya kukihamasisha kizazi kipya cha wamisionari. Wakati akiwa Korea kusini , kwa mfano , aliwatangaza kuwa watakatifu wamisionari 124 waliosaidia kupeleka imani hiyo katika eneo la rasi ya Korea.

Pia amezungumzia mara kwa mara juu ya mashahidi wa zama hizi, Wakristo katika mashariki ya kati na Afrika ambao wameuwawa na wanamgambo wa Kiislamu.

Uganda Papst Franziskus mit Präsident Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni akionesha ishara ya kumkaribisha papa FrancisPicha: Reuters/S. Rellandini

Historia ya mashahidi wa Uganda imesaidia kuelekeza kanisa la Katoliki nchini Uganda, wakati idadi kubwa ya mahujaji wakimiminika katika eneo hilo la Namugongo, wengi wao wakiwa Waafrika wanaowasili kutoka mbali kama Congo an Tanzania . Wengi wa mahujaji wanatembea masafa marefu hadi katika eneo hilo kuimarisha imani yao.

Makao makuu ya kanisa hilo hayakusema iwapo Francis atajadili haki za mashoga akiwa nchini humo.

Siku ya Jumapili , Francis anakwenda katika kituo chake cha mwisho katika ziara hii ya Afrika , katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Issac Gamba