1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedikt XVI ashangiriwa Freiburg

Martin,Prema/dpa25 Septemba 2011

Nchini Ujerumani, takriban vijana 30,000 wameshiriki katika misa ya jioni iliyosomwa na Papa Benedikt wa 16 katika mji wa Freiburg.

https://p.dw.com/p/Rnci
Papst Benedikt XVI. feiert am Donnerstag (22.09.11) im Olympiastadion in Berlin eine Messe. Foto: Thomas Lohnes/dapd
Papa Benedikt XVIPicha: dapd

Hapo kabla, maelfu ya waumini walimshangiria kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alipokuwa ndani ya gari lake maalum kuelekea kwenye Kanisa la Freiburger Münster. Papa Benedikt vile vile alikuwa na mkutano wa faragha pamoja na kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl, aliesifiwa kwa jitahada zake katika kuleta muungano wa Ujerumani.

Katika mkutano wake na viongozi wa Kanisa la Orthodox, Papa Benedikt alitoa mwito kwa wakristo wote kushirikiana pamoja kukabiliana na mwelekeo wa kupinga dini, unaokutikana katika jamii.