Pakistan yasitishwa uwanachama wa Jumuiya ya Madola | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Pakistan yasitishwa uwanachama wa Jumuiya ya Madola

Jumuiya ya Madola ya nchi wanachama 53 imesitisha uwanachama wa Pakistan katika jumuiya hiyo hapo jana baada ya Rais Pervez Musharrafa wa Pakistan kushindwa kuondowa utawala wa hali ya hatari nchini mwake na kujiuzulu ukuu wa majeshi kufikia muda wa mwisho aliowekewa na jumuiya hiyo.

Jumuiya ya Madola ilimpa Mushrraf hadi jana kuondowa utawala wa hali ya hatari aliouweka hapo tartehe 3 mwezi wa Novemba.

Musharraf alikuwa ameanza kuregeza baadhi ya vipengele vya utawala wa hali ya hatari na maafisa wa serikali ya Pakistan wanasema ataapishwa kama kiongozi wa kiraia siku mbili hizi baada ya mahkama kuu hapo jana kuondowa pingamizi ya mwisho ya kisheria iliokuwa inapinga uhalali wa kuchaguliwa tena kuwa rais.

Wiki hii Musharraf aliwaachilia mahabusu waliokuwa wakishikiliwa tokea tarehe 3 mwezi wa Novemba na pia ameahidi kufanya uchaguzi wa bunge tarehe nane Januari.

Kundi la Utekelezaji la Jumuiya ya Madola la ngazi ya mawaziri lililopewa jukumu la kuangalia upya uwanachama wa Pakistan limesema hali nchini Pakistan inaendelea na ukiukaji mkubwa wa maadili ya msingi ya kisiasa ya jumuiya hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Don McKinnon akisoma taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kampala ambapo mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola unafanyika amesema kwamba Pakistan inasitishwa uwanachama wa jumuiya hiyo mara moja hadi hapo demokrasia na utawala wa sheria utakaporudishwa nchini humo.

 • Tarehe 23.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CS9m
 • Tarehe 23.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CS9m

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com