Pakistan yapewa siku 10 kurejesha katiba | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Pakistan yapewa siku 10 kurejesha katiba

Wazir mkuu wa zamani wa Pakistan, Benazir Bhutto amesema,hatoshiriki tena katika majadiliano ya kugawana madaraka pamoja na Musharraf.Amesema,hawezi kufanya kazi pamoja na mtu anaeondosha katiba na kukandamiza mahakama.

Benazir Bhutto akizungumza na mwandishi wa habari mjini Lahore

Benazir Bhutto akizungumza na mwandishi wa habari mjini Lahore

Bhutto,kwa mara nyingine tena amewekwa katika kizuizi cha nyumbani katika mji wa mashariki wa Lahore.Serikali imesema,hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu ya kuwepo vitisho vya kutaka kumuua.Lakini chama cha Bhutto cha Pakistan People´s Party kinasema,azma ni kumzuia kuongoza maandamano ya kupinga hali ya hatari iliyotangazwa na Rais Pervez Musharraf Novemba 3.

Kwa upande mwingine,Jumuiya ya Madola imeipa Pakistan muda wa siku 10 kurejesha katiba ya nchi na kuondosha hali ya hatari.Isipofanya hivyo itafukuzwa kutoka Jumuiya ya Madola.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com