1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

OSLO:Mkutano wa kupiga marufuku mabomu ya kutawanyika waendelea Norway

Mkutano wa kimataifa unaojadilia athari za mabomu ya kutawanyika cluster bombs unafunguliwa mjini Oslo nchini Norway hii leo.Wawakilishi kutoka mataifa 40 wanahudhuria mkutano huo unaolenga kupiga marufuku matumizi ya mabomu hayo yanayosababisha vifo vingi vilevile kulemaza hasa raia wa kawaida.Mambomu ya kutawanyika husambaa kama vipande vidogo vya bomu katika eneo kubwa jambo linaloyafanya kuwa hatari sana.

Kulingana na Umoja wa Mataifa mambomu hayo yanapatikana katika mataifa 21 ambayo ni sawa na mabomu milioni 33 madogo.Makundi ya kutetea haki za binadamu kwa upande wao yanasema kwamba idadi hiyo haipaswi kuruhusiwa kuongezeka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com