1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olimpik na vyombo vya habari

29 Julai 2008

China ilipogombea kuandaa Olimpik 2008 iliahidi kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari:

https://p.dw.com/p/Elzo

Michezo ya olimpik ya majira ya kiangazi itafunguliwa rasmi August 8-kiasi cha wiki kutoka sasa.

"Ijumaa ya tareje 13" si siku ya bahati mbaya kama baadhi walivyo nas itikadi ya siku hiyo. Mjii wa Beijing, ulifurahia na kusherehekea siku hiyo ya ijumaa,Julai 13, 2001.

Siku hiyo miaka 7 hivi iliyopita,Halmashauri Kuu ya olimpik Ulimwenguni ikikutana mjini Moscow, ilitangaza kuwa michezo ya olimpik ya majira ya kiangazi 2008 itafanyika beijing.

Na sio tu kwa kuwa China iliahidi vituo maridadi kwa michezo hiyo,mandhari za kijani kimazingira bali pia kulinda haki za binadamu.

Hata uhuru wa magazeti na vyombo vya habari uliahidiwa kuhifadhiwa na China endapo ikikubaliwa kuandaa michezo hiyo. Je, china sasa imetimiza ahadi hizo ?

►◄

Jiang Xiaoyu ni mtu mwenye madaraka makubwa nchini china.Yeye ni makamo-rais wa Kamati ya Maandalio ya michezo ya olimpik ya Beijing, 2008.

Pale mwezi Machi, mwenge wa olimpik ulipokumbana na maandamano makali takriban katika kila mji wa nchi ya magharibi ulikopita,alisikika akisema , michezo ijayo ya olimpik itakua ya kispoti tu na haitachanganishwa na siasa.

Miaka 7 nyuma pale Beijing ilipoania kuandaa michezo hii, sauti nyengine kabisa ilisikika.

Wakati ule Beijing binafsi iligombea michezo hiyo ikiambatanisha na siasa na hivyo ikafanikiwa: Diwani mkuu wa jiji la beijing Liu Jingmin alisema hjapo Februari 2001, kugombea kuandaa michezo ya olimpik sio tu kuhimize maendeleo ya jiji linaloandaa, bali hata maendeleo ya jamii.

Hii inajumuisha pia demokrasi na haki za binadamu.

Na pia julai 12,2001 siku moja kabla beijing haikuteuliwa kuandaa michezo ijayo,makamo-mwenyekiti wa Kamati yake ya maandalio ya olimpik Wang Wie kuwa:

vyombo vya habari vikija china kwa michezo ya olimpik,vitakuta uhuru kamili wa kuripoti.

Paul Steiger,ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama kinachowalinda waandishi habari (CPJ) kutoka Marekani.Mnamo mwaka uliopita alijishughulisha mno na vyombo vya habari vya China .Kuhusu ahadi zilizotolewa wakati ule anasema:

"Ahadi zilizotolewa hadharani ni uhakikisho tangu wa Halmashauri kuu ya Olimpik ulimwenguni (IOC) hata China

ni kuwa -vizuwizi vilivyowekewa vyombo vya habari vitaregezwa katika muda wote wa michezo hii ya olimpik.Na hii inaingiza kipindi kinachoelekea michezo na wakati wa michezo yenyewe na baadae."

Kusema kweli, vikwazo viliregezwa ,lakini kwa waandishi habari kutoka nje ya china tu.Kuanzia Januari mosi,2007 waandishi kutoka nje wamepewa uhuru wa kufanya taftishi zao China nzima bila pingamizi.Kufanya mahojiano ilihitaji ridhaa tu ya yule anaefanyiwa.Na hii ikarahisisha mno kazi ya muandishi habari wa kigeni.

Hatahivyo, Jocelyn Ford ripoti yake ina kasoro nyingi.Ford anatumika kama muandishi anaejitegemea mjini Beijing.Katika klabu ya waandishi-habari wa kigeni ya China, jukumu lake ni kuchungua iwapo kuna uhuru kweli wa vyombo vya habari.Anasema:

" Mwaka 2007,mwaka wa mwanzo kutolewa muongozo huo wa kuwapa waandishi habari wa kigeni uwanja huru wa kuripoti,mwongozo huo ulikiukwa mara 180.Baadhi ya wanachama wetu walihujumiwa.Na wengi wakizuiliwa katika kazi zao wanapofanya mahojiano na machina.Ni serikali iliozuwia mahojianohayo.tumewahi kuwa na hali ambamo waandishi habari wa kigeni wakiandamwa moja kwa moja.

Wanafanyiwa kero tangu kupatiwa hati za ruhusa maalumu ili kuwazuwia wasiripoti visa walivyopanga kuripoti.Na hivyo kutoweza kufanya kazi zao.Tunajionea kuingiliwa mno katika kazi zetu za kuripoti."

Alisema Jocelyn Ford.

Ni jana tu China ilipokanusha tuhuma za shirika linalotetea haki za binadamu ulimwenguni-Amnesty International kuhusu mashtaka ya kukiuka kwa haki za binadamu:

Msemaji wake wa wizara ya nje Liu Jianchao alisema kwamba, yeyote aijuae China hatakubaliana na ripoti ya shirika linalotetea haki za binadamu na wafungwa wa kisiasa-Amnesty International.

Ripoti ya Amnesty iliilaumu china kwa kushindwa kutimiza ahadi zake ilizotoa kuheshimu zaidi haki za binadamu katika kipindi cha kuielekea michezo ya wiki ijayo ya olimpik mjini Beijing.

Amnesty ilidai kuwa serikali ya China imewatia nguvuni maalfu ya wananchi wanaodai mageuzi pamoja na wakereketwa wa haki za binadamu mwaka jana.Liokadai kuwa hiyo ni kampeni ya serikali ya Beijing kuusafisha mji wa Beijing kabla ya michezo ya olimpik kufunguliwa.