1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olimpik Beijing

Ramadhan Ali8 Agosti 2007

Michezo ya 29 ya olimpik ya Beijing 2008 inatazamiwa kuipüiku kwa mavuno zaidi ya fedha ile ya Seoul,1988 na hata Barcelona 1992.

https://p.dw.com/p/CHbQ

China inaanza leo kuhesabu mwaka kamili hadi itakapofungua michezo ya 29 ya Olimpik ya majira ya kiangazi ya 2008 mjini Beijing.

China imearifu kwamba matayarisho yote yanakwenda sawa sawa ingawa kuna hofu na wasi wasi juu ya hali ya hewa kutokana na kuchafuka kwa mazingira. Na ingawa hakuna awezae kutabiri itakuaje mwakani wiki kama hii,China imeahidi kuchukua hatua ya kusafisha anga lake ili wanariadha wake kwa waume, waweze kuvuta pumzi sawa sawa.

China haipangi tu kuipiku Marekani na kuibuka dola litakalonyakua medali nyingi kabisa za dhahabu,fedha na shaba, bali kama Marekani 1984, huko Los Angeles, inapanga pia kutia faida nono kutokana na michezo hii ya olimpik.

Kama Korea ya kusini 1988 na Spain,1992,China imetia raslimali kubwa ya fedha katika kuandaa michezo hii.Na inataka pia kuvuna inachopanda hivi sasa tangu kispoti hata kiuchumi.

Isitoshe, China inataka kupitia michezo ya Olimpik kutembeza mila na utamaduni wake, maendeleo yake ya kisasa iliofanya.Imekisia kwamba gharama yake huenda ikafikia Euro bilioni 30.

Prof.Jin Yuanpu wa chuo kikuu cha “peoples University” anatamaa kubwa kwamba raslimali China inayotia itavuna matunda yake.

Beijing na China nzima zinajikuta wakati huu katika kipindi cha mpito.Nchi yetu inapiga hatua za maendeleo katika kila sekta.Michedzo hii ya olimpik imechangia nguvu zaidi katika maendeleo yetu tangu ya kijamii hata ya kiuchumi na kutupa fursa kubwa za kujiendfeleza.”

Hatahivyo, prof.huyo anaungama kwamba kupitia michezo ya olimpik mchangao wake katika ukuaji wa uchumi wa China hautazidi 1%.Uchunguzi wa Banki ya raslimali ya JP Morgan unasema michezo ya Olimpik haitachangia chochote kusukuma gurudumu la maendeleo ya uchumi wa China .Kwani, uchumi wa china bila ya michezo hii unasonga mbele na kustawi.

Hatahivyo, inatarajiwa michezo ya Beijing katika sekta ya biashara itaipiku michezo yote iliopita hadi sasa:Pekee haki za kuionesha michezo hii katika TV zimepanda mno kuliko wakati wowote.Vyombo vya habari vya China vinataja ni dala bilioni 1.7.Kituo cha TV cha Marekani cha NBC kimenunua haki za TV kwa bei ya dala milioni 9000.

Nafasi ya pili kwa kulipa kima cha juu ni Umoja wa Radio wa Ulaya.Nusu ya mapato hayo yanakwenda katika mfuko wa Halmashauri ya maandalio ya michezo hii ya olimpik ya China.51% ya fedha hizo zinakwenda mfukoni mwa mashirika ya kispoti ya kimataifa na kwa IOC-Halmashauri Kuu ya Olimpik Ulimwenguni.

Miongoni mwa wafadhili wakuu wa michezo ya Beijing ni makampuni 3 makubwa ya Ujerumani: Schenker,Adidas na kampuni la magari Volkswagen.

Rupert Stadler,mjumbe wa bodi ya AUDI-tawi la VW asema:

“Kupitia tafrija kadhaa za kispoti na kitamaduni, tutatembeza magari yetu ya AUDI nchini China .Kwa mara ya kwanza tumetoa magari 1000 kuhudumia wagenikatika safari zao na hii ni barabara kabisa.”

Asema mjumbe huyo wa AUDI.

Kampuni la zana za michezo la ADIDAS ndilo linalowavika mavazi wajumbe wa Olimpik na timu ya wanariadha wa China.

Kwahivyo, michezo ya Beijing sio tu itakua ya kuvunja rekodi uwanjani bali hata viwandani.