1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Odinga autaka Umoja wa Afrika usimtambue rais Kibaki

25 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cxbl

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Rail Odinga, leo ameutaka Umoja wa Afrika usitambuje kuchaguliwa tena kwa rais Mwai Kibaki kufuatia uchaguzi uliokumbwa na visa vya udanganyifu na wizi wa kura.

Odinga amesema viongozi wa Umoja wa Afrika watakaokutana kuanzia tarehe 31 mwezi huu hadi tarehe mbili mwezi ujao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, wasimtambue Kibaki kama rais wa Kenya na usimruhusu atume ujumbe kuhudhuria mkutano huo.

Umoja wa Afrika Jumanne wiki hi ulilaani kile ilichokiita ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchiniKenya kufuatia uchaugzi wa mwaka jana na kutaka uchunguzi ufanywe.

Sambamba na hayo, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amefutilia mbali uwezekano wa kcuhukua wadhifa wa waziri mkuu katika serikali itakayoongozwa na rais Kibaki.

Baadhi ya vyombo vya habari na wanadiplomasia wamependekeza hiyo inaweza kuwa njia mojawapo ya kuutanzua mgogoro wa kisiasa nchini Kenya.