1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama ziarani London

24 Mei 2011

Rais Barack Obama wa Marekani amewasili London mapema kuliko ilivyopangwa, baada ya kubadilisha ratiba ya ziara yake kutokana na kitisho cha majivu ya mlima wa Volkano, Grimsvötn, huko Iceland.

https://p.dw.com/p/11MZA
Rais Barack Obama
Rais Barack ObamaPicha: AP

Rais Obama anaitembeleas London kutokana na mwaliko wa malkia Elisabeth wa pili wa Uengereza.Amepangiwa pia kukutana na waziri mkuu David Cameroun.Baadae ataelekea Deauville nchini Ufaransa kuhudhuria mkutano wa kilele wa mataifa manane tajiri kiviwanda-G-8 kabla ya kwenda Poland kituo cha mwisho cha ziara yake ya siku sita barani Ulaya.

Ziara ya mjini London ni kilele cha kwanza cha ziara ya rais Barack Obama barani Ulaya,ingawa amekwishafika mara kadhaa,lakini, hii ni ziara yake ya kwanza rasmi.Rais Barack Obama na mkewe Michelle watakaribishwa kwa shangwe na hishma za kijeshi na Malkia Elisabeth wa pili na mumewe mwanamfalme Philip katika kasri la Buckingham wanakotazamiwa kusalia wakati wote wa ziara hii ya siku tatu mjini London.Wamepangiwa pia kukutana kwa muda mfupi na mwanamfalme William na mkeweCatherine.Leo usiku malkia Elisabeth wa pili ameandaa karamu rasmi kwaajili ya mgeni wake wa kutoka Marekani na mkewe.

Ingawa rais Barack Obama amepangiwa pia kukutana na waziri mkuu David Cameron hii leo,lakini kitovu cha mazungumzo ya kisiasa ni kesho,atakapokutana tena na waziri mkuu David Cameron na hasa pale rais Obama atakapohutubia mabaraza yote mawili ya bunge la Uengereza.Msemaji wa rais Obama,Jay Carney anasema:

"Hotuba yake itamulika kile rais Obama alichokilenga katika ziara yake hii yaani kushadidia uhusiano wa kipekee pamoja na washirika wa Ulaya na hasa katika ziara yake hii rasmi mjini London,kutilia mkazo uhusiano mahsusi uliopo pamoja na wananchi wa Ufalme wa Uengereza."

NATO Angriffe auf Tripolis Libyen Gaddafi
Mashambulio ya NATO mjini TripoliPicha: dapd

Rais Obama atakuwa kiongozi wanne kuhutubia mbele ya mabaraza yote mawili ya bunge la Uengereza,baraza la wawakilishi na baraza la Senet,tangu vita vikuu vya pili vya dunia,baada ya Charles de Gaule mnamo mwaka 1960,Nelson Mandela mwaka 1996 na kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni,Benedikt wa 16 mnamo mwaka 2010.

Hii leo ,mnamo siku ya kwanza ya ziara yake mjini London,rais Barack Obama alilitembelea eneo yanakokutikana mabunge yote mawili ya Uengereza huko Westminster na kuweka shada la mauwa juu ya kaburi la askari mwanajeshi asiyejulikana.

Mada za maasilahi ya pamoja hazijakosekana,kuanzia Afghanistan kupitia Libya ,mapambazuko katika ulimwengu wa kiarabu hadi kufikia juhudi za amani katika Mashariki ya kati.

Katika wakala wao wa pamoja kupitia gazeti la The Times,rais Barack Obama na waziri mkuu David Cameron wametilia mkazo " uhusiano wa kimsingi kati ya nchi hizi mbili."Uhusiano wetu sio tu ni uhusiano maalum ,bali ni uhusiano muhimu kwetu na kwa ulimwengu kwa jumla-wamesema viongozi hao wawili.

Mwandishi: Paulert Rüdiger (WDR) /Hamidou Oummilkheir/,afp

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman