1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama strebt Neubeginn mit dem Iran an

Nina Markgraf20 Machi 2009
https://p.dw.com/p/HGHa
Rais wa Marekani Barack Obama.Picha: AP / DW-Fotomontage


Wakati ni sasa kwa Iran kuchukua nafasi yake muhimu katika jamii ya mataifa. Katika mojawapo ya matamshi muhimu aliyotoa katika utawala wake mchanga, Rais Barack Obama alisema Marekani iko tayari kuikaribisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kujumuika na jamii ya mataifa  iwapo Iran itapokea mualiko. Mjini Tehran, rais Mahmoud Ahmedinajad anasemekana ameukaribisha msimamo huu mpya wa Marekani, lakini kwa tahadhari. Marekani kwanza lazima iponeshe vidonda kati yake na Iran.



Iwapo ulimwengu ulikuwa na walakini kuwa Marekani, chini ya Rais Obama, imepania kuwa na sura tofauti kutoka ile ya Bush, katika kukabiliana na mahasimu wao....mkono wa utawala huu mchanga unaounyooshea kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huenda itaondoa tashwishi zozote.


'' Utawala wangu uko tayari kuikaribisha jamhuri ya kiislamu ya Iran kuchukua nafasi yake muhimu katika jumuiya ya Mataifa, Ndio lilikuwa ombi la rais Obama alipowatakia heri njema watu wa iran Ijumaa hii, siku yao ya kusherehekea sikukuu ya Nowruz, au mwaka mpya nchini Iran.



''  Nyinyia pia muna uamuzi. Marekani inaitaka Jamhuri ya kiislamu ya Iran kuchukua nafasi yake muhimu katika jumiya ya mataifa. Muna haki hiyo. Lakini pia inakuja na majukumu yake, nafasi hii haiwezi kupatikana kwa kutumia vitendo vya ugaidi au silaha....lakini inapatikana kwa vitendo vya amani vinavyoashiria watu wa Iran ni watu wenye hadhi kuu. Na kuonyesha hadhi yenu kuu, ni kupitia kujenga wala si kubomoa .'' Ndivyo Obama alisema katika ukanda wa video.


'' Sherehe hizi ni mwanzo mpya. Kwa miongo miatau uhusiano kati ya nchi zetu hizi mbili umekuwa mbaya, lakini sikukuu hii itatukumbusha kuwa sote ni watu wenye kupenda utu...na hilo ndilo litatuweka pamoja. Aliendelea kusema Obama.


Tangu mwaka 1980 uhusiano wa wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran ulikatizwa.

Mjini Tehran, Rais Mahmoud Ahmedinejad alisema amepokea ombi hili kutoka kwa Obama, lakini akaongeza Tehran kwanza inataka Marekani ichukue hatua kubwa kulainisha makosa dhidi ya Iran.


Kulingana na mshauri mkuu wa Ahmedinejad, nia ya Obama ya kutaka mabadiliko ni sharti iandamwe na matendo wala si maneno tu. Iran imeshikilia msimamo kuwa Marekani ndiyo iliyoanza kuibughudhu Iran. Mfano waliotoa ya madhara Marekani iliwafanyia raia wa Iran..ni vile vita vya Iran na Iraq pale Marekani ilipomuunga mkono Saddam Hussein.


Marekani nayo daima imekuwa ikiishtumu Tehran kwa juhudi zake za kutaka kutengeza mradi wa kinukliya. Obama pia hajaacha msimamo kuwa Iran lazima isite kuunga mkono makundi ya kigaidi au yenye siasa kali.


Dalili kwamba uhusiano kati ya Marekani na Iran huenda ukaimarika zilianza kuonekana pale Washington ilipoialika Iran kuhudhuria kongamano la kimataifa kuhusu Afghanistan mwisho wa mwezi huu. Iran imesema itaangilia iwapo itaukubali mualiko huo.


Mwandishi:Munira Muhammad/ AFP

Mhariri:  Miraji Othman