1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama awa mshindi.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkF3

Iowa, Marekani. Nchini Marekani gavana wa zamani Mike Huckabee ameshinda katika utaratibu wa kwanza wa uteuzi katika jimbo la Iowa kwa chama cha Republican, akiwashinda wapinzani maarufu katika kura hizo za kwanza za uteuzi kwa uchaguzi mkuu wa rais mwaka huu. Ushindi huo wa Iowa unampa Huckabee, ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Arkansas , nguvu na utambulisho kitaifa wakati akielekea katika kura ya uchaguzi mwingine wa uteuzi hapo Januari 8 katika jimbo la Hampshire.

Katika uchaguzi wa uteuzi kwa chama cha Democratic, Barack Obama ameibuka mshindi, akipata asilimia 38 za kura. Seneta huyo kutoka jimbo la Illinois amewaambia kundi la watu waliokuwa wakimshangilia kuwa Wademocrats wanatoa ujumbe mzito kuwa mabadiliko yanakuja sasa nchini Marekani.

John Edwards alimaliza akiwa wa pili na Hillary Rodham Clinton amemaliza wa tatu.