1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama atuma kikosi cha washauri wa kijeshi Uganga

15 Oktoba 2011

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa anapeleka kikosi cha washauri wa kijeshi 100 nchini Uganda kusaidia majeshi ya eneo hilo yanayomsaka kiongozi wa LRA Joseph Kony.

https://p.dw.com/p/12sRz
Rais wa marekani Barack Obama ametuma kikosi cha wanajeshi nchini Uganda.Picha: dapd

Katika barua kwa baraza la Congress jana Ijumaa, rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa anapeleka kiasi washauri wa kijeshi 100 nchini Uganda kusaidia majeshi ya eneo hilo ambayo yanamtafuta Joseph Kony pamoja na makamanda wengine wa kundi la Lord's Resistance Army, LRA. Obama amesema kuwa ameidhinisha idadi ndogo ya wanajeshi kusaidia kumuondoa kiongozi huyo wa Lord's Resistance Army kutoka eneo la mapambano. Hata hivyo amesema, licha ya kuwa kikosi hicho kitakuwa na silaha lakini wanajeshi hao watatoa tu taarifa, ushauri na msaada kwa majeshi ya mataifa washirika.