1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama akutana na viongozi wa Israel na Palestina

Kalyango Siraj23 Julai 2008

Asema ziara yake hii inatilia mkazo uhusiano kati ya Marekani na Israel

https://p.dw.com/p/EiSl
Seneta Barak ObamaPicha: AP/DW

Seneta Baraka Obama ambae anagombania kwenda Ikulu ya Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrat yuko mashariki ya kati na tayari amekutana na Marais wa Israel pamoja na Palestina.

Miongoni mwa yale aliyotamka katika eneo hilo, ni kuahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu kati ya Marekani na Israel endapo atafanikiwa kwenda ikulu ya Washington.

Barak Obama akiwa katika ziara yake ya siku mbili mashariki ya kati amemwambia kiongozi wa mamlaka ya Palestina, Mahmood Abbas,kuwa ikiwa atachaguliwa kama rais wa Marekani atakuwa mshirika wa maana na ataharakisha kuingilia mgogoro wa eneo hilo.

Mkutano wao wa saa moja ulikuwa katika makao makuu ya serikali ya Bw Abbas yanayopatikana Ramallah katika eneo la Ukingo wa magharibi.

Alipokuwa Jordan Obama alionya kuwa si sawa kutaraji kuwa rais wa Marekani pekee anaweza kuleta amani katika eneo hilo mara moja.

Lakini hapo awali akiwa mjini Jerusalem Obama akikutana na rais Shimon Perez mjini Jerusalem aliahidi kuiunga mkono Israel kwa udi na uvumba na kulielezea taifa hilo la kiyahudi kama muujiza.

A kiwa huko amewambia maripota kuwa nia ya safari yake hii ni kukariri uhusiano maalum kati ya Marekani na Israel na pia azma yake ya kuona kama nchi hiyo inalindwa.Maneno hayo yanafanana kama yale aliyoyatoa nchini Marekani akihutubia jamii ya wahayudi ambapo alisisitiza kuwa mji w Jerusalem ni lazima ubaki mji mmoja na kuwa mji mkuu wa taifa la Israel

Neno kuhusu Jerusalem liliwashangaza sana viongozi wa Palestina.Wapalestina wanataka sehemu ya mji wa Jerusalem ya mshariki ambayo ni ya waarabu iliotekwa na Israel mwaka wa 1967 kuwa mji mkuu wa taifa la Palestina.Baadae Obama alisema kuwa alitumia maneneo yasiofaa wakati huo.

Obama alichukua mda mrefu katika ardhi ya Israel kuliko ya Palestina.

Aidha amekutana na waziri wa Ulinzi wa Israel Ehud Barak pamoja na kiongozi wa upinzani Benjamin Netanyahu.

Pia ametembelea mji wa mpaka wa Israel na Ukanda wa Ghaza unaosimamiwa na kundi la Hamas wa Sderot ambao kila mara unashambuliwa na makombora ya wapalestina.

Mpinzani wake wa chama cha Republican John McCain nae mwezi wa Machi alifika katika mji huo,lakini hakwenda katika ukingo wa magharibi wa wapalestina.

Baadae Obama amepangiwa kukutana na waziri wa mashauri ya kigeni Tzipi Livni pamoja na waziri mkuu Ehud Olmert.

Aidha Seneta Obama alivaa kibagarashio cha wayahudi na kuweka shada la maua katika sehemu ya makumbusho ya mauaji ya halaiki ya Holokosti.