1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama aja Ujerumani

24 Aprili 2016

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuwasili mjini Hanover, nchini Ujerumani leo Jumapili (24.04.2016) na kuwa na mazungumzo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

https://p.dw.com/p/1IbZb
England Besuch US Präsident Obama beim Town Hall Meeting
Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: Getty Images/AFP/J. Tallis

Merkel, ni mmoja kati ya washirika wa karibu wa rais Obama katika kupambana na uchumi wa dunia unaoyumba pamoja na mizozo ya kiusalama katika mashariki ya kati na Ukraine.

Kitakuwa kituo chake cha mwisho katika ziara ya siku sita katika mataifa ya kigeni ambako Obama ametaka kuimarisha ushirika wa Marekani na mataifa washirika mataifa anayoyaangalia kuwa ni muhimu kukuza uchumi, kulishinda kundi la dola la Kiislamu, na kudhibiti mabavu ya Urusi nchini Ukraine na Syria.

Deutschland Barack Obama und Angela Merkel in Baden-Baden
Barack Obama na kansela Angela Merkel(kulia)Picha: Getty Images/S. Gallup

Obama, ambaye yuko katika miezi yake tisa ya mwisho katika muhula wake wa mwisho wa urais, amekuwa kwa siku tatu mjini London ambako amewataka Waingereza kuchagua kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni itakayofanyika mwezi Juni, kura ambayo inaweza kuleta msituko katika uchumi wa dunia.

Maonesho ya biashara

Mapema wiki hii, alikutana na viongozi wa mataifa ya ghuba mjini Riyadh kujaribu kupunguza hofu kwamba Marekani imepunguza msisitizo wake kuhusiana na usalama wao.

Deutschland Demonstration gegen TTIP und CETA in Hannover
Wapinzani wa makubaliano ya kibiashara kati ya Marekani na mataifa ya Ulaya TTIPPicha: DW/S. Kinkartz

Mjini Hanover, atazuru na kuzungumza katika maonesho makubwa ya biashara na Merkel. Viongozi hao wanataka kuweka uhai katika makubaliano kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya ya biashara huru ambayo wale wanaoyaunga mkono wanasema yataweza kuongeza uwezo wa uchumi wa kila upande kwa kiasi cha dola bilioni 100.

Msukumo wake unakuja katika wakati ambapo watu wengi wa Ulaya na Marekani kwa pamoja wanatia shaka kwamba makubaliano hayo yanaweza kugharimu kazi zao na kuathiri viwango.

Deutschland Hannover Proteste gegen TTIP
Waandamanaji wakiingia mitaani mjini HanoverPicha: Getty Images/AFP/J. Macdougall

Makubaliano ya kibiashara

"Lakini muda haumsubiri yeyote katika wakati huu," amesema Heather Conley, afisa wa zamani wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani katika enzi za utawala wa rais George W. Bush, hivi sasa akiwa katika kituo kwa ajili ya mikakati na mitaala ya kimataifa mjini Washington.

Deutschland Hannover Proteste gegen TTIP
Waandamanaji mjini HanoverPicha: Getty Images/AFP/J. Macdougall

Viongozi wanajaribu kukamilisha mazungumzo tata kuhusu ushirika wa uwekezaji na biashara katika eneo la mataifa hayo yanayotenganishwa na bahari ya Atlantic yaani TTIP kabla Obama, kutoka chama cha Democratic, kuondoka madarakani Januari 20.

Obama anatokea Uingereza kuja Ujerumani ambako amesema katika mahojiano yaliyotangazwa leo Jumapili na shirika la utangazaji la BBC kwamba makubaliano ya kibiashara kati ya Uingereza na Marekani yanaweza kuchukua miaka mitano hadi kumi kujadili iwapo Uingereza itapiga kura kujitoa katika Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni itakayofanyika Juni 23.

Deutschland G7 Gipfel Barack Obama und Angela Merkel Schloss Elmau
Obama(kushoto) akizungumza na kansela Merkel(kulia)Picha: picture-alliance/dpa/V. Mayo

Ziara ya Obama na uamuzi ya kuingilia kati katika majadala wa Umoja wa ulaya umeukasirisha upande wa kampeni ya kujitoa, ambayo imekuwa ikidai mara kwa mara kwamba Uingereza inaweza kirahisi kujadili makubaliano na kupata masharti mazuri zaidi ikiwa nje ya Umoja huo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Bruce Amani