1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyuma ya Maikrofoni - Vyombo vya Habari

12 Agosti 2013

Je, umewahi kujiuliza vipindi uvipendavyo vya redio au televisheni vinatengenezwa vipi? Sasa Noa Bongo inakupa fursa ya kufahamu vyema yote yanayotokea kabla ya kutazama televisheni au kusikiliza vipindi katika redio.

https://p.dw.com/p/19Nzv
Mwanamke anashika redio na kusikiliza (Picha: DW)
Picha: DW

Waandishi wa habari hutuletea habari kemkem kuhusu kashfa mbalimbali, kukutana na watu mashuhuri na pia huwa hawakosekani mahali popote jambo linapotokea. Uandishi wa habari ni taaluma nzuri na ya kusisimua - lakini pia inayozungukwa na vihoja vyake. Na hiyo ndio hali inayokumba sekta ya usanii.

Mfano nchini Nigeria, sekta ya filamu inazidi kuimarika kila kukicha huku maelfu ya waigizaji wakibadilika na kuwa watu mashuhuri maishani. Lakini bado watu wengi hawafahamu ugumu wa kuwa muigizaji.

Hii ni fursa nzuri ya kujifunza mengi kuhusu ulimwengu wa habari kupitia vipindi vya Noa bongo vinavyoangazia sekta hii ya vyombo vya habari. Katika vipindi hivi tutachunguza yale yanayoendelea wakati wa utayarishaji wa vipindi.


Kutana na Young Junior, Sister P, Charlie na Ezra, vijana kutoka Afrika, katika mfululizo wa vipindi kumi, kwenye mchezo huu wa redio, wanapojifunza mengi wanayohitaji kuyafahamu kabla ya kuanzisha kituo cha redio na kukiendeleza. Pia utasikia yote kuanzia umuhimu wa kudumisha maadili ya uandishi wa habari hadi kufikia kiwango cha kutangamana na watu mashuhuri .

Vipindi vya Noa Bongo Jenga Maisha Yako vinasikika katika lugha sita: Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Kiamhara. Na kufadhiliwa na wizara ya nchi za kigeni nchini Ujerumani.