1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nuri al-Maliki nchini Marekani.

23 Julai 2009

Waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki ameliomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kufuta madeni nchi yake inailipa Kuwait kama fidia .

https://p.dw.com/p/Ivn6
Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki wakiwahutubia waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani.Picha: AP

Rais wa Marekani, Barack Obama, amesema kuwa amemshinikiza waziri mkuu wa Iraq, Nuri al Maliki, kutoa nafasi katika serikali yake na katika idara ya ulinzi kwa makabila yote pamoja na madhehebu ili kuzuia kutokea tena ghasia ambazo karibu zisababishe vita vya wenyewe kwa wenye katika nchi hiyo.

Akiapa kutimiza ahadi ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq itimiapo mwaka 2011, rais Obama amesema yeye pamoja na waziri mkuu wa Iraq, Nuri al Maliki, walikubalina kuwa bado hakuna utulivu nchini Iraq na kutakuwa na wakati mgumu katika siku za usoni. al-Maliki yuko nchini Marekani ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu rais Obama angie madarakani mwezi Januari mwaka huu.

Wakiwa katika Ikulu ya Marekani mjini Washington, rais Obama alisema kuwa Marekani na Iraq ziko kwenye mkondo wa kuhakikisho kuwepo mabadiliko nchini Iraq. Rais Obama alisema kuwa huu ndio wakati wa kuboresha uhusiano ambao umekuwepo kati ya Marekani na Iraq wakati wa miaka sita ya vita nchini humo.

Ghasia zinaendelea kupungua nchini Iraq na Wairaq wanachukua jukumu la kuboresha hali katika siku za usoni. Hatua zimepigwa na wananchi wa Iraq pamoja na vikosi vya usalama, wakiwemo wanajeshi wa Marekani. Sasa hivi tuko katika harakati za kuleta mabadiliko na ushirikino kati ya Mareikani na Iraq pamoja na kuheshimiana. Ufanisi wa mabadiliko haya ni ajenda kuu katika utawala wangu,Alisema rais Obama.

Matamshi ya rais Obama ni ishara kuwa utawala wake una lengo la kuvimaliza vita vya Iraq na kuuangazia zaidi mzozo uliopo nchini Afganistan. Wanajeshi wa Marerklnai waliivamia Iraq mwaka 2003 kumng'oa madarakani rais Saddam Hussein na hadi sasa wanajeshi 130,000 wa Marekani bado wamesalia nchini humo kusaidia kuilinda nchi hiyo na pia kuwapa mafunzo wanajesui wake.

Hadi sasa wanajeshi wa Marekani 4,300 wameuawa katika vita hiyvo, huku maelfu ya Wairaq pia wakiuawa na wengiine mamilioni kukikimbia makwao katika vita hivyo vilivyodumu muda wa miaka sita. Iraq, Iliyo na utajiri wa mafuta, sasa inahitaji fedha za kujijenga upya baada ya miaka kadha ya vikwazo pamoja na vita.

al-Maliki anasema kuwa huu ni wakati mwafaka wa uwekezaji wakati usalama unaendelea kushuhudiwa, lakini, hata hivyo, matamshi yake yanafanywa kukiendelea kushuhudiwa ghasia. Jana, jumatano, wanamgambo waliwaua watu watano waliokuwa kwenye basi, siku moja baada ya mabomu kuripuka mjini Baghadad na kuuwa watu 16.

al-Maliki ataka Iraq kufutiwa fidia inayoilipa Kuwait.

Wakati huo huo, al-Maliki ameliomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kufuta madeni nchi yake inatakiwa kuilipa Kuwait kama fidia ya vita.

Mwaka 1991, wakati wa vita vya Ghuba, baraza la usalama la umoja wa mataifa liliiamrisha Iraq ilipe fidia kwa nchi zilizoathirika na vita wakati Iraq iliidhibiti Kuwait. Hadi sasa Iraq inatenga asillimia tano ya pato lake la mafuta kwa fidia hiyo, kiasi kikubwa kikipelekwa Kuwait.

Ziara hiyo ya wiki moja anayofanya al-Maliki nchini Marekani ina lengo la kuashiria kujitegemea kw Iraq, na kuwahimiza wawekezaji kurejea tena nchini humo. Pia kuuishinikiza umoja wa mataifa kufuta deni inayolipa kwa mataifa mengine.

Mwandishi :Jason Nyakundi/RTRE

Mhariri :Othman Miraji