1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

November tisaa katika ahistoria ya Ujerumani

Oummilkheir8 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7ex
Ukuta wa zamani wa Berlin
Ukuta wa zamani wa BerlinPicha: picture-alliance/ dpa

November tisaa ni tarehe muhimu katika historia ya hivi karibuni ya Ujerumani.Ni siku inayokumbusha fadhaa na furaha kwa wakati mmoja,ni siku ambayo wanatzi walaitia moto mahekalu,maduka na milki nyenginezo za wayahudi hata kabla ya vita vikuu vya pili kuanza –Progromnacht na pia siku iliyoshuhudia kuporomoka ukuta wa Berlin mnamo mwaka 1989.Si hayo tuu November tisaa ilikua tarehe ya kumalizika enzi za ufalme na kutangazwa jamhuri ya kwanza ya Ujerumani mwaka 1918 na njama ya Hitler kuipindua jamhuri miaka mitano baadae,yote hayo yamefungamana na November tisaa.

November tisaa inakamilika miaka kumi tangu ukuta wa Berlin ulipoporomoshwa.Tukio lililoibadilisha sura nzima ya dunia.Hapakufika hata mwaka baadae,October tatu mwaka 1990,Ujerumani ikaungana upya baada ya kutengana kwa miaka 41.Kwa kutoweka enzi ya pili ya kiimla katika ardhi ya Ujerumani,kwa kutoweka GDR,ikafutika pia kambi ya ujamaa katika ramani ya Ulaya.Mgogoro kati ya kambi ya mashariki na kambi ya magharibi ukamalizika.November tisaa mwaka 1989 ikageuka siku ya majaaliwa katika historia ya Ujerumani na Ulaya kwa jumla.

Katika kalenda ya historia ya wajerumani,November tisaa ina maana nyingi muhimu.Mwaka 1918,Philip Scheidmann wa kutoka chama cha Social Democratic,akisimama katika dirisha la jingo la Reichtags (bunge la wakati ule),alitangaza kuundwa jamhuri ya Ujerumani.Ni tarehe iliyomaliza enzi za ufalme wa Kaisari Wilhelm wa pili .

“Wafanyakazi na wanajeshi,tambueni umuhimu wa kihistoria wa siku hii ya leo.Kuna kilichotokea.Kuna kazi kubwa isiyokadirika inayotusubiri.Yopte kwaajili ya wananchi-yote kupitia wananchi.Hakuna linalobidi kutokea ambalo linachafua hadhi ya vuguvugu la wafanyakazi.Muwe kitu kimoja,watiifu na waadilifu.Utawala mkongwe na potovu wa kifalme umetoweka.Enzi mpya imeibuka-naiishi jamhuri ya Ujerumani.“

Demokrasia changa ya Ujerumani ilianza kukumbwa na misuko suko tangu mwanzo.Wafuasi wa mrengo wa shoto na wale wa mrengo wa kulia walitaka kuipiga kumbo haraka iwezekanavyo.November tisaa mwaka 1923,wazalendo wa kijamaa wakaivamia kambi ya kijeshi ya mjini München.Kiongozi wao alikua Adolf Hitler ambae miaka kumi baadae alikuja kutwaa ,kwa njia iliyokua halali, hatamu za uongozi nchini Ujerumani na kuutumbukiza ulimwengu mzima katika balaa kubwa kupita kiasi:vita vikuu vya pili vya dunia.

Katika njia yake kuelekea katika janga hilo,wayahudi nchini Ujerumani walianza kidogo kidogo kupokonywa haki zao,kabla ya kuteketezwa moja kwa moja katika mwaka 1942.November tisaa mwaka 1938,mwaka mmoja hivi kabla ya vita vikuu vya pili vya dunia kuripuka,masenagogi ya wayahudi yakaanza kutiwa moto kote nchini Ujerumani,na maduka ya wayahudi kuvunjwa na mali kuporwa.Wayahudi kama mia hivi wakauliwa na 26 elfu wakapelekwa katika kambi za maangamizi.Janga hilo la masinagogi na maduka kutiwa moto ,wanazi wakalipa jina la kejeli-„Usiku wa vigae.“Ilikua kama zowezi jumla la mpango mzima wa mauwaji ya halaiki ya wayahudi Holocaust.

November tisaa mwaka 1938 ni miongoni mwa tarehe za msiba mkubwa.Kinyume na November tisaa mwaka 1989,siku ambayo ukuta uliporomoka.Hakuna aliyeamini!Neno moja tuu ndilo lililokua midomoni siku ile usiku„ Doo -Haiwezekani“-habari zilipoenea kwamba ukuta wa Berlin umeporomoka na mipaka ni wazi kwa wakaazi wa GDR.Ingawa miezi kadhaa kabla ya hapo maandamano yalipamba moto dhidi ya utawala wa wakongwe katika makao makuu ya chama tawala cha SED Berlin Mashariki.Maelfu walikimbilia Hungary na katika ofisi za Shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Ulaya ya mashariki.Kishindo cha kuwarahisishia vibali vya kusafiri wakaazi wa Ujerumani mashariki kilizidi siku hadi siku.Hakuna lakini aliyeamini :Mkutano pamoja na waandishi habari wa kimataifa ulipoitishwa Berlin Mashariki kupunguza mara moja vizuwizi vya watu kusafiri-hakujaakua tena na kizuwizi:Maelefu kwa maelfu walivuka mpaka wa Berli-Furaha iliyoje

„Hivi punde tuu waliwaachia baadhi wapite ,baadae wakalidfungua lango.Hatuhitaji kuonyesha kitambulisho,tunatoka bila ya chochote.Bila ya kukaguliwa.Hata kitambulisho sina.“

Hakujakua tena na kurudi nyuma baada ya tarehe hiyo.Tobo la kwanza katika ukuta wa Berlin likapelekea kuporomoka mfumo mzima wa Ujerumani mashariki ya zamani.Na kwa mara ya nne November tisaa ikaingia katika madaftari ya historia ya Ujerumani.Safari hii kwa furaha.