1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOUKCHOUT : Wananchi wa Mauritania wapiga kura

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKH

Wananchi wa Mauritania wameanza kupiga kura leo hii katika uchaguzi wa rais wa kihistoria kukamilisha kurudisha madaraka kwa utawala wa kiraia kufuatia mapinduzi wa kijeshi hapo mwezi wa Augusti mwaka 2005.

Upigaji kura ulianza saa moja asubuhi na unatazamiwa kumalizika saa 12 jioni katika vituo vya kupiga kura 2,400 vilivyotawanyika katika nchi hiyo nzima ya jangwa ya jamhuri ya Kiislam yenye idadi ya watu milioni tatu.

Misururu ya wapiga kura imeonekana katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Zaidi ya watu milioni moja wanastahiki kupiga kura kumchaguwa rais mpya katika uchaguzi huo unaoadhimisha hatua ya mwisho kuirudisha nchi hiyo katika utawala wa kidemokrasia wa kiraia baada ya mapinduzi ya kijeshi kukomesha miaka 20 ya utawala wa kidikteta wa Maaouiya Ould Taya.