1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOUADHIBOU.Wahamiaji wasio halali kurejeshwa makwao

13 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSm

Meli iliyokuwa imewabeba watu 370 wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji wasio halali wenye asili ya kiafrika na kiashia imetia nanga katika bandari ya Nouadhibou nchini Mauritania.

Inaaminika kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea katika visiwa vya Canary nchini Uhispania wakati ilipoharibika.

Maafisa wa usalama wa Uhispania waliikamata meli hiyo wiki moja iliyopita.

Watu hao watarudishwa makwao kwa mujibu wa taarifa za utawala wa Uhispania.