1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOUACKCHOTT: Uchaguzi huru baada ya utawala wa kijeshi

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK6

Wapiga kura nchini Mauritania,siku ya Jumapili, wamepiga kura kumchagua rais mpya katika uchaguzi huru wa kwanza wa rais baada ya nchi hiyo kuwa na utawala wa kijeshi kwa miongo kadhaa.Upigaji kura ulikwenda kwa usalama nchini humo,ambako kiasi ya watu milioni 1.1 wana haki ya kupiga kura. Wagombea 19 wamepigania kura katika uchaguzi unaotarajiwa kumaliza utawala wa kijeshi katika nchi ambako uongozi haukubadilishwa kwa njia ya uchaguzi tangu miaka 47.Utaratibu wa kuleta mabadiliko ulianzishwa baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2005 yaliyofanywa bila ya mmuagiko wa damu.