1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni nani Muktada al-Sadr

Sekione Kitojo
15 Mei 2018

Alijulikana  kama mwanamgambo anayepambana  na  Marekani, mwanamageuzi  katika pande zote  za  madhehebu ya  dini  na matumaini  mapya  kwa  Iraq. Muktada al-Sadr ni nani katika siasa za Iraq?

https://p.dw.com/p/2xlTc
Irak, Bagdad: Portrait Muqtada al-Sad
Picha: picture-alliance/K. Kadim

Kutoka  kupigana  vita  dhidi  ya  vikosi vya  jeshi  la  Marekani  hadi  kushinda  kwa  kiwango  kikubwa katika  uchaguzi, DW  inaangalia  hatua  za  mabadiliko  za  Muqtada al-Sadr. 

Akiunganisha  Waislamu  wa  madhehebu  ya  Shia  na  jamii zisizo na  dini chini  ya  kauli  mbiu  ya  mageuzi, ushindi  wa  al-Sadr katika  uchaguzi  unaashiria  kilele  cha  miaka  ya  kazi  zinazolenga kupambana  na  rushwa  pamoja  na  ubadhirifu  katika  serikali. Lakini al-Sadr  alijenga  jina  lake  katika  kila  kitu  lakini  bila  ya kuingia  katika  siasa  za  nchi  hiyo. Wakati vuguvugu  lake  la kisiasa  lilivuka  mipaka  ya  kimadhehebu  kwa  kubadilishana  na jukwaa  la uzalendo, kiongozi  huyo  wa  kidini  wa  Shia  ana historia  ya  ndani  sana  ya  kuimarisha  migawanyiko  hiyo.

Irak, Bagdad: Radikale Shiiten ehren Majid Kassim
Wanamgambo wa al-Sadr nchini IraqPicha: picture-alliance/K. Kadim

Hakuna  mtu  yeyote  aliyefikia  kuwa  kielelezo  cha  mapambano dhidi  ya  uvamizi  wa  Marekani  kama  al-Sadr. Juni mwaka  2003, aliunda  jeshi  la  lililovuma  kwa  ubaya  la  Mahdi kama  njia  ya kupambana  na  siku  moja  kuyafurusha  majeshi  ya  uvamizi.

"Sadr  aliweka  wazi  kwa  matamshi  yake  na  kusema  kwamba alikuwa  kwanza  kabisa  ni  mzalendo  wa  Iraqi, ambaye  hadhibitiwi na  mataifa  yenye  nguvu  ya  kigeni, iwe  Iran, Marekani  ama  nchi nyingine  yoyote,"  alisema Thanassis Cambanis  wa Wakfu  wa Century  wa  kukusanya  mawazo  wiki  iliyopita.

Mapambano  na  majeshi  ya  Marekani

"Matokeo  yake , na  hususan   katika  miaka  ya  mwanzo   baada ya  uvamizi, Sadr alikuwa  mmoja  wa  makamanda  wachache  wa wanamgambo  ambaye  alipata  heshima  japo  ya  mbali  kutoka makundi  yote  ya  kimadhehebu."

Irak Parlamentswahlen Plakat von Muqtada al-Sadr bei Feier auf dem Tahrir-Platz
Wafuasi wa kiongozi wa kidini wa Iraq Muqtada al-Sadr Picha: picture alliance/AP/H. Mizban

Lakini wanamgambo  vijana  wa kiongozi  huyo  wa  kidini walibakia kwa  kiasi  kikubwa  chini  ya  uangaliazi  hadi  mwaka  2004, wakati walipopambana  na  vikosi  vya  majeshi  ya  Marekani  katika  mji wa  kusini  wa  Najaf, na  kusababisha  kampeni  kubwa  iliyowalenga wanajeshi  wa  Marekani  nchini  humo.

Mwaka  huo , majeshi  ya  Marekani  yaliamuriwa  kumtafuta  na kumkamata  akiwa  hai  ama  amekufa  baada  ya  jaji  wa  Iraq kutoa  waranti  wa  kukamatwa kwa  mauaji  ya  wanajeshi  wa Marekani.

Kwa  rais  wa  zamani  wa  Marekani George W. Bush , vitendo  vya al-Sadr  na  wafuasi  wake  vilifikia  katika  kile   alichosema  kuwa ni  kupinga  demokrasia.

Jeshi  la  Mahdi  halikuwalenga  tu wanajeshi  wa  Marekani. Katika kipindi  chake  cha  mapambano , wanamgambo  hao  pia waliwalenga  Wairaqi  wa  madhehebu  ya  Sunni na  makundi mengine  ya  Washia. Jeshi  hilo  lilishutumiwa  kwa  kufanya  mauaji kwa  kuunda  vikosi  vya  mauaji , na  kwa  kufanya  hivyo wakachochea  mivutano  ya  kimadhehebu.

Irak, Bagdad:  Proteste bewaffneter Militanten
Wapiganaji wa jeshi la Mahdi likiongozwa na Muqtada al-SadrPicha: picture-alliance/K. Kadim

Iliofika  mwaka  2006 , jarida  la  habari  la  Marekani Newsweek lilimuweka  al-Sadr  katika  ukurasa  wa  mbele  na  kumpa  jina  la "mtu  hatari  zaidi  nchini  Iraq."

Kundi  hatari  zaidi

"Kundi  hilo  lilikuja  kuangaliwa  katika  maeneo  mengi  ya  Iraq kuwa  hatari  zaidi  kuliko  kundi  la  al-Qaeda  nchini  Iraq  na la  pili kwa  vikosi  vya  Marekani  kwa  uwezo  na  nguvu  za kijeshi,"  kwa  mujibu  wa  mradi  wa  kuangalia  maeneo  ya wanamgambo  katika  chuo  kikuu  cha  Stanford.

Hata  hivyo , jeshi  la  Mahdi  lilianza  kupoteza  uungwaji  mkono mwaka  2007 , baada  ya  mahujaji  wa  Kishia  50  kuuwawa  katika mapambano  na  kundi  jingine  la  wanamgambo  wa  Kishia  katika eneo  la  Karbala. Mwaka  uliofuatia , al-Sadr  aliamuru wanamgambo  wake  kuweka  silaha  zao  chini. Wakati  baadhi  ya wapiganaji  walichukuliwa  kuingia  katika  jeshi  la  serikali, wengine walipewa  jina  la  Mumahidoon  na  kuelekeza  nguvu  zao  katika huduma  za  jamii  kama  masomo  ya  Qurabi, ujenzi  katika halmashauri  na  kukusanya taka  katika  maeneo  ya  Washia.

Arabische Emirate, Abu Dhabi:  Arabischer Kronprinz trifft sich mit  Muqtada Al-Sad
Mwanamfalme kutoka Abu Dhabi akikutana na Muqtada al-SadrPicha: picture alliance/R. Carter

Mwaka  2008 , al-Sadr alikwenda  Iran, ambako  alibaki  huko  akiishi uhamishoni. Hata  hivyo , aliendelea  kuongoza vuguvugu  la  Sadr na  kutumia  mamlaka  yake  kushawishi hali  ya  kisiasa  nchini  Iraq.

Mwaka 2011, al-Sadr  alirejea  nchini  Iraq  ili  kuwa  na  usemi mkubwa  katika  siasa  za  nchi  hiyo. Mwishoni  mwa  mwaka  huo , majeshi  ya  Marekani  yalikamilisha  kujitoa  nchini  Iraq, na kukamilisha  dai  kuu  la al-Sadr.

Mwandishi: Kersten Knipp / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman