1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Ngangari", "mdosi" na "kipute" yanamaanisha nini?

29 Juni 2011

Katika Baraza hili la Msamiati, mtaalamu wa lugha wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle, Othman Miraji, anazungumza na wanazuoni wa lugha ya Kiswahili juu ya asili, maana na matumizi ya maneno kama "mdosi" na "kipute".

https://p.dw.com/p/RWTb
Othman Miraji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle
Othman Miraji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche WellePicha: DW

Sauda Barwani: "Neno 'ngangari' lilianza kutumika kwenye mikutano ya kisiasa, likimaanisha 'kakamaa', likiwa na lengo la kuwatia watu hamasa".

Omar Babu: "Mtu akisema yuko ngangari, anakusudia kuwa yuko imara....yuko thabiti!"

Mtayarishaji/Muongozaji: Othman Miraji

Washiriki/Wataalamu: Omar Babu (Chuo Kikuu cha Cologne), Sauda Barwani (Chuo Kikuu cha Hamburg), Profesa Abdulatif Abdalla (Chuo Kikuu cha Leipzig)