NEW YORK:Waziri wa nje wa Tanzania achaguliwa kua naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:Waziri wa nje wa Tanzania achaguliwa kua naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa

New-York:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania,Dr. Asha Rose Migiro amechaguliwa kua naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa.Akitangaza uamuzi huo,katibu mkuu Ban Ki-Monn amesema Dr. Migiro anastahiki sana cheo hicho,amedhihirisha ujuzi na ustadi wa kusimamia shughuli za uongozi na amekua daima akiyatetea mataifa yanayoendelea.Katibu mkuu Ban Ki-Monn anasema atamkabidhi Dr. Asha Rose Migiro sehemu kubwa ya shughuli za uongozi na utawala,pamoja na masuala ya uchumi jamii na maendeleo.Bwanas Ban aliyekabidhiwa wadhifa wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa january mosi iliyopita,alikwishasema hapo awali,atamkabidhi waadhifa wa naibu katibu mkuu mwanasiasa wa kike kutoka ulimwengu wa tatu .Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania anaehudhuria mkutano wa kimkoa hivi sasa nchini Lesotho,anatazamiwa kuwasili makao makuu ya Umoja wa mataifa wiki ijayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com