NEW YORK:UN yalaani nia ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 20.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:UN yalaani nia ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameitaka Israel kufikiria upya uamuzi wake wa kulitangaza eneo la Ukanda wa Gaza kuwa ni eneo hatari.

Serikali ya Israel imesema kuwa itakata huduma ya nishati ya umeme kwenda eneo hilo la Ukanda wa Gaza, ikiwa ni kulipa kisasi kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya maroketi yanayofanywa na wanamgambo wa kipalestina.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleza Rice aliye ziarani Mashariki ya Kati ametetea uamuzi huo wa Israel.

Amesema kuwa Marekani inalichukulia kundi la Hamas kuwa ni kundi hatari na adui.

Hamas kwa upande wake limeilaumu Israel kwa hatua hiyo likisema ni kutangaza vita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com