NEW YORK:Uchunguzi ufanywe kuhusu ghasia za nchini Kongo | Habari za Ulimwengu | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:Uchunguzi ufanywe kuhusu ghasia za nchini Kongo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon na wajumbe wa Baraza la Usalama wametoa wito wa kufanywa uchunguzi kuhusu ghasia zilizotokea juma lililopita nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Zaidi ya watu 100 waliuawa katika machafuko yaliozuka kwenye jimbo la Bas Kongo.Katibu Mkuu Ban ametoa wito wa kusitisha machafuko hayo moja kwa moja na msaada wa kiutu kutolewa kwa wahanga na familia zao.Hapo awali,Ban alisifu kuundwa kwa serikali mpya nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,miezi sita baada ya kufanywa chaguzi za bunge.Serikali ya waziri mkuu Antoine Gizenga ilitangazwa mjini Kinshasa juma lililopita.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemhimiza Gizenga kutenzua matatizo ya usalama nchini Kongo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com