1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Mameya watoa mwito wa kupambana na joto

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0z

Mameya kutoka miji 30 ya dunia wamezitaka nchi nane tajiri duniani ziongeze juhudi katika kupambana na ongezeko la joto duniani.

Mameya hao wamesema hayo katika azimio walilopitisha mwishoni mwa mkutano wao mjini New York

Mameya hao wametoa mwito huo wakati ambapo viongozi wa nchi tajiri nane wanajitayarisha kukutana nchini Ujerumani mwezi ujao.