NEW-YORK:Baraza la usalama la UN lalaani mashambulio dhidi ya Bhutto | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW-YORK:Baraza la usalama la UN lalaani mashambulio dhidi ya Bhutto

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga la wiki iliyopita dhidi ya msafara wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto mjini Karachi.

Baraza la usalama limelitaja shambulio hilo kuwa kitendo kiovu cha kigaidi.Katika taarifa baraza hilo la usalama lenye wanachama 15 limezitolea mwito nchi zote kushirikiana katika kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na kitendo hicho.Halikadhalika baraza hilo limesisitiza kwamba litafanya kila liwezalo kupambana na ugaidi wa aina yoyote duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com