1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Vikwazo dhidi ya Iran bado havijafikiwa

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChK

Wanachama watano wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani wamemaliza mazungumzo bila kufikia makubaliano juu ya vikwazo dhidi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia.

Baada ya mkutano wa wajumbe kutoka Marekani, Urusi, Ufaransa, Uingereza, China na Ujerumani, mjumbe wa Urusi, Vitaly Churkin, amesema mambo kadhaa bado hayajasuluhishwa. Churkin amesema azimio litatayarishwa na kupigiwa kura hapo kesho.

Mapendekezo ya vikwazo yaliyotayarishwa na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza yanajumulisha kupigwa marufuku kwa usafiri na kuzuiliwa kwa mali za wairan wanaohusika katika mpango wa nyuklia wa nchi yao.